Tz 216 ELCT Nkuhungu Student Centre

Home Contact Guest Book

 

 

HISTORIA FUPI YA HUDUMA YA MTOTO

 
 

Kuanzishwa Kwa Huduma. Kuanzishwa kwa huduma hii ni kuiunga mkono juhudi za serikali yetu ya kumjengea mazingira mazuri Mtanzania aweze kuondokana na ujinga, maradhi na umaskini uliokithiri miongoni mwa Watanzania. Na zaidi ni kumnasua mtoto kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa umaskini, maradhi na ujinga pamoja na fikira potofu za kujidharau, kujiona mnyonge asiyeweza kitu chochote.

Ili kumjengea mtoto mazingira mazuri na uwezo katika maisha ya kiroho, kiafya, kielimu na kiuchumi aweze kuwa raia mwema mwenye kumjua na kumtegema Mungu katika maisha yake yote. Awe Mkristo mtu mzima mwenye kujisimamia, kuwajibika na kujitosheleza katika maisha yake na jamii na kuwa viongozi bora katika Kanisa, Taifa na Kikazi chao.

HALI YA HUDUMA HADI SASA. Hadi leo tarehe 14/03/2008 kituo kina jumla ya watendakazi 4 nao ni kama ifuatavyo;1.   Ndugu Godbless Kissanga –Mratibu 2.    Ndugu Hagary Kimaro -  Mhasibu 3.      Ndugu Neema Swallo -  Social Worker 4.      Ndugu Atupyanie Matimbwi -  Health worker

  • HITIMISHO LA HISTORIA YA HUDUMA.

Kama Kanisa linawajibika kusimama na kutembea katika haki na uaminifu katika kumuinuwa mtoto huyu muhitaji na kumpandisha katika nuru ya utukufu wa Mungu ambayo ndiyo matunda pekee anayohitaji Mungu.

Pia ni wajibu wa Kanisa kuduisha na kusitawisha upendo, heshima, mshikamano wa kidungu, mioyoni mwa watendakazi, watoto, Wazazi na walezi wao, na miongoni mwa kamati mbalimbali zinazoweza kusaidia kumzalia Mungu matunda mema kwa kumtunza mtoto huyu na kusimamia haki yake ipasavyo.Tunamshukuru Mungu na tunamwomba atuwezeshe kutimiza utume  na wajibu huu kwa unyenyekevu, unyofu uadilifu na uaminifu siku zote hata ajapo tena.

Imeandaliwa na  Kituo cha:-

HUDUMA YA MTOTO TZ 216 ELCT NKUHUNGU

 
 

Previuos Page   

 
Copyright © 2007 GKISSANGA All rights reserved.