Tz 216 ELCT Nkuhungu Student Centre
|
HISTORIA FUPI YA HUDUMA YA MTOTO |
UANDIKISHAJI WATOTO KUJAZA NAFASI Tarehe 30/09/2003 CIT ilituruhusu kujaza mapengo ya watoto waliofariki, walio hama na walio futwa kwenye Huduma hii kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo familia husika kuwa na uwezo wa kuwalea watoto wenyewe, na wengine kuto fuata mashariti ya Huduma. Hivyo tuliweza kujaza mapengo hayo kwa kuongeza watoto wapya 12.Pia tarehe 18/06/2007 CIT walitoa kibali cha kuongeza watoto wengine 40 ambao walifanya kituo kuwa na jumla ya watoto 270. MAFANIKIO – BARAKA Hivyo kufikia leo hii tarehe 14/03/2008 tuna jumla ya watoto 265 wanao hudumiwa hapa Kanisani.Watoto wetu tangu wameandikishwa wanajifunza masomo mbalimbali kama Neno la Mungu, Masomo ya afya, Michezo mbalimbali, Utunzaji wa mazingira pia wanakuwa na safari mbali mbali za mafunzo. Watoto 130 kati ya watoto tulio nao walipata Biblia zao tarehe 12/05/2007. Tunamshukuru Mungu watoto wanazingatia masomo mashuleni na masomo ya afya pia, kwani wanaendelea kuwa wasafi na wenye afya nzuri. Wengi wao wanajua kusali na wengi kubadirika kitabia kuacha uchokozi wamekuwa na upendo na furaha kubwa na hasa tunapowatembelea nyumbani kwao. KAMATI YA HUDUMA YA MTOTO Katika huduma hii ya mtoto pia tuna kamati ambayo ilichaguliwa ili kuweza kuongoza na kusimamia huduma hii ya mtoto. Kamati hii imeonyesha ushirikiano na moyo wa kumtumikia mtoto na tunamshukuru Mungu na awabariki sana kwa kujitoa kwao. WALIMU WA SHULE YA BIBLIA Tunamshukuru Mungu kituo hiki kina walimu 8 amboa wanawafundisha watoto shule ya Biblia kila siku ya Jumamosi. Ni walimu ambao wamepata mafunzo mbalimbali kupitia semina mbalimbali zilizo andaliwa na CIT ili kuwapatia ujuzi na uzoefu wa kufundisha katika huduma hii kwa ufanisi mzuri. KUSUDI LA HUDUMA “Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaezekee baba zao, ili nisije nikapiga dunia kwa laana” Malaki 4:6 Kwa kuzingatia ujumbe huu wa Mungu ni budi pawepo na matengenezo makubwa yanayohitaji gharama kubwa na muda wa kutosha. Kusudi kuu la kuanzishwa huduma hii hapa kanisani ni ili kujenga, kuimarisha na kudumisha mahusiano ya familia ambapo hapo penye kipimo cha kumwalika Mungu ashushe Baraka zake. Ni kukiunda kizazi kipya ambacho kitamtii Mungu na kumtegea Mungu daima. |
|