Tz 216 ELCT Nkuhungu Student Centre
|
HISTORIA FUPI YA HUDUMA YA MTOTO |
SEMINA YA KUSHIRIKISHANA MAONO – VISION SHARING Tarehe 05/08/2007 kulifanyika semina ya kushirikishana maono juu ya huduma ya Compassion juu ya mtoto. Vision Sharing iliyofanyika CCT Dodoma, na washiriki wa semina walikuwa watendakazi watatu walichaguliwa, kamati ya Huduma ya mtoto, viongozi wa kanisa na waalimu watakaofundisha watoto neno la Mungu. UANDIKISHAJI WATOTO – CHILD SCREENING Tarehe 09/08/2008 Uongozi wa kanisa ulifuatilia kuomba kibali cha serikali kwa afisa Mtendaji wa Kijiji ili kuruhusiwa kupita nyumba kwa nyumba.Ndipo tarehe 12/hadi 15/08/2002 zoezi la uandikishaji watoto nyumba kwa nyumba zoezi hilo lilifanyika na liliongozwa na Mchungaji Kiongozi Mch. Jackson Shalua akisaidiana na watendakazi wa Kituo cha Huduma ya mtoto wa kanisa la AICT kizota chini ya usimamizi wa watumishi toka CIT Ndugu Jackson Mollel na Ndugu Enock Kijo. Tarehe 15/08/2002 zoezi lilikamilika kwa kupata watoto 230 toka familia wahitaji na mitaa iliyotembelewa ni Mtube, Chingali West, Kizota, Salama Mbwanga na Chang’ombe. SEMINA KWA WATENDA KAZI WAPYA Tarehe 27/08/2002 mpaka tarehe 21/09/2002 ilifanyika Semina kwa watendakazi wote wa vituo vipya vya Huduma ili kuwapatia ujuzi na uwezo wa kumhudumia mtoto. Semina ilifanyika kanisa la Moravian Arusha Road.Makanisa yaliyoshiriki katika Semina hiyo yalikuwa kama ifuatavyo:1. Anglican Chang’ombe (Mradi No. 310) 2.Anglican Msalato (Mradi No. 311) 3.FPCT Nkuhungu (Mradi No. 809) 4. Menonite Iringa Road (Mradi No 701) 5. ELCT Nkuhungu (Mradi No 216)6.TANG AICC (Mradi No.114) 7.Moravian Arusha Road (Mradi No 550) KUANZIA HUDUMA RASMI KANISANI Tarehe 24/08/2002 watoto walianza rasmi kukutana pamoja kwa huduma ya Neno la Mungu pamoja. MATATIZO NDANI YA HUDUMA. Kuondokewa kwa Mchungaji.Tarehe 03/03/2007 mchungaji wetu Isaac Makanta aliitwa na Bwana na kuzikwa hapa Dodoma tarehe 07/03/2007 |
|