Tz 216 ELCT Nkuhungu Student Centre
|
HISTORIA FUPI YA HUDUMA YA MTOTO UTANGULIZI “Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie; kwa maana watoto wadogo kama hawa ufalme wa Mungu ni wao’’ MARKO 10:13-14. Mikakati ya ufalme wa Mungu inafundishwa na kuelezwa katika maandiko matakatifu na kufananishwa ya maisha ya mtoto mdogo; jinsi anavyoonekana na kufahamika na Mungu. Ni tofauti na mtazamo wa mwanadamu anayemuona mtoto ni kama kitu cha baadaye. Kwa kuzingatia ujumbe huo wa mungu, Huduma hii inatekeleza kusudi kuu la Bwana la kumuongoza na kumpeleka mtoto kwa Yesu. Mtoto amepewa nafasi ya kwanza kuonyesha kwamba wokovu ni kwa watu wote wa Mataifa yote na wa hali zote na marika yote. Hivyo basi kwa heshima tunaelezea historia ya mwanzo ya utekelezaji wa kusudi kuu la Bwana wetu Yesu Kristo la kumpeleka mtoto kwa Yesu hapa kanisani. Kwa ushirikiano mkuu wa kifamilia kati ya Compassion International Tanzania na Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa nkuhungu - Dodoma; iliadhimia kumuandaa mtoto kwa maisha ya hapa Duniani, na baadae uzima wa milele mbinguni kwa Mungu Baba, tukizingatia pia ujumbe wa Mungu kwamba. “Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee” MITHALI 22:6 MWANZO WA HUDUMA TZ 216 ELCT – NKUHUNGU KUPATIKANA KWA WATENDA KAZI Baada ya mawasiliano na watumishi wa CIT na kupata kibali kwamba Kanisa lina sifa ya kupokea na kuwatunza watoto. Hivyo yalifanyika makubaliano na maelewano rasmi tarehe 24/07/2002 kati ya uongozi toka CIT na Mch. Jackson A. Shalua kwa niaba ya uongozi wa Dayosisi.Ndipo Huduma hii ilipoanza rasmi tarehe 24/07/2002 ikiwa ni jumla ya watoto 230 ambao waliandikishwa kupitia nyumba kwa nyumba.Tarehe 27/07/2002 ulifanyika usaili kwaajili ya kupata watendakazi ambao watahudumia watoto usahili uliosimamiwa na wajumbe wa Kanisa na watumishi toka CIT. Ndipo tarehe 28/07/2002 matokeo ya usaili yalitanganzwa Kanisani wale waliochaguliwa kushika Huduma hii takatifu ya Mungu walikuwa 1.Mrs.Hagary Kimaro -Alipendekenzwa awe Mratibu 2.Mr.Emmanuel S. Niniko- Nafasi ya Mhasibu na 3. Miss Neema Swallo- Nafasi ya Social Worker |
||