USHUHUDA WA MTOTO

Home Contact Guest Book

 

       
       
 

USHUHUDA WA MTOTO ELLY DICKSON MWAKALUKWA (TZ-216-0215)

Mtoto huyu alizaliwa tarehe 01/01/1996 kwa sasa yuko Form Three katika shule ya SEKONDARI CHINANGALI- DODOMA TANZANIA.

Ufuatao ni ushuhuda wake mwenyewe alio uandika tarehe 02/06/2010

Kwa jina naitwa Elly Dickson Mwakalukwa. Kabila langu ni Mnyakyusa. Nilizaliwa tarehe 01/01/1996.

Baba na mama ( Wazazi wangu ) walifariki kitambo nikiwa bado ni mdogo sana. Kwa sasa ninaishi na Bibi yangu mzaa Baba pamoja na dada yangu. Namshukuru Mungu sana kwa kunitunza hadi hapa nilipo fikia. Baba na mama walipo fariki, nilipata bahati ya kuandikishwa katika kituo cha Huduma ya mtoto kilichopo KKKT Usharika wa Nkuhungu ( TZ-216 ELCT NKUHUNGU STUDENT CENTRE) Kwa kweli Kituo hiki kimefanyika baraka sana katika maisha yangu.

Ninakishukuru sana kituo hiki kwa mambo makubwa kilicho nitendea hadi hapa nilipo fikia. Nikiwa hudumani niliugua ugonjwa wa Homa ya UTI WA MGONGO, kituo kiliweza kunisaidia sana katika matibabu yangu kwa kuniuguza hadi sasa ni mzima wa afya njema na sina ulemavu wa aina yoyote. Hili ni jambo jema sana na sina budi kumshukuru Mungu na kumrudishia sifa na tukuzo yeye peke yake wa kuabudiwa.

Mimi nimeokoka na ninampenda Yesu kwani ni Bwana na mwokozi wa maisha yangu. Namshukuru Mungu pia kwa kunipa vipawa mbalimbali vikiwemo vya kuomba na uimbaji.Kwa sasa ni mwenyekiti wa kwaya ya kituo TGC ( Talentesd Gosple Choir) na ndie mmoja wapo wa ma sollolist wa kwaya hii.

Ninamuahidi Mungu kulitangaza jina lake mahali popote nipatapo nafasi na kuyasimulia matendo yake makubwa na yaajabu aliyo nitendea kwangu binafsi na hata kwa familia yangu kwa ujamla. Jina la Bwana libarikiwe

Ni mimi Mtoto Elly Dickson Mwakalukwa.

 
  Back to previous page  
Copyright © 2008 GKISSANGA All rights reserved.