USHUHUDA WA MTOTO

Home Contact Guest Book

 

       
       
 

USHUHUDA WA MTOTO JACQULINE MICHAEL SANGA (TZ-216-0008)

Mtoto huyu alizaliwa tarehe 12/08/1994 kwa sasa yuko darasa la SABA katika shule ya MSINGI NKUHUNGU- DODOMA TANZANIA.

Ufuatao ni ushuhuda wake mwenyewe alio uandika tarehe 22/03/2008

Kwa jina naitwa Jacquline Michae Sanga ninamshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa nilipo sasa. Bila ya Mungu mimi nisingeweza kuwa hapa nilipo. Nakumbuka siku walipo pita waalimu kuandikisha watoto walinikuta nikiwa nyumbani pamoja na mama yangu.

Waalimu walimuambia mama yangu wanaandikisha watoto ambao wanishi katika mazingira magumu. Mama yangu akasema hadi amwambie mjomba wangu kwanza. Waalimu wakamueleza mama basi akiwa tayari aende katika kanisa la KKKT  Nkuhungu.

Siku ilifuatia mama alikuwa bado hajaonana na mjomba. Mimi nikamuomba aende akaniandikishe na mama aliniambia kama naweza niende mwenyewe. Niliondoka mwenyewe nyumbani na kwenda Kanisani KKKT ndipo nilipo ambiwa niende na kadi ya kuzaliwa.Ikabidi niifuate kadi nyumbani na mama akanipa. Nilipo kuja nayo waalimu waliniambia hadi nije na mzazi wangu. Nikarudi kumuaelza mama na mama akaniambia hawezi kwenda kwani wanasumbua tuu. Nakumbuka jirani yetu pia alikuwa amemuandikisha mtoto wake ndiye aliye mweleza na kumshawishi mama aniandikishe.

Siku iliyo fuata tuliondoka na mama kwenda kuniandikisha nakumbuka siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho. Zamu yetu ilipo fika mama alijieleza na ndipo nilipo andikishwa. Baada ya kuandikishwa tuliendelea kwenda kila siku Jumamosi kujifunza Neno la Mungu.

Kuwapo Kituoni nimejifunza mambo mengi kwanza nimejuana na watu wengi na kujipatia marafiki wengi sana. Nimetembelea uwanja wa ndege, nimetembelea Bwawa la Hombolo na sehemu nyingine nyingi.  Nimepata matibabu kila nikiugua tena natibiwa bure. Nimejifunza ushonaji vitambaa, utengenezaji wa Batick na hadi sasa mie nacheza timu ya Netball ya Kituo.

Toka niingie kituoni mwaka 2002 nimepata mabadiliko mengi. Nilikuwa sijui usafi ni nini? Kwa kwenda semina mbalimbali nimeweza kujifunza kitu ambacho nilikuwa sijui. Nilikuwa sijui neno la Mungu na jinsi ya kumpenda mungu na kupendani sisi kwa sisi lakini sasa najiua.. Nimepata mfadhili ambae pia tuna andikiana barua kila wakati. Ananipenda na mie ninampenda sana pia huwa ananitumia zawadi mara kwa mara..

Ninamshukuru sana Mungu kwa Kituo kunifikisha hapa nilipo kwani kama nisinge andikishwa ningeweza kuwa mtoto wa mitaani maana hata kumjua Mungu au kupendana sisi kwa sisi ningekuwa sijui.

Ni mimi Mtoto Jacquline Michael Sanga.

 
  Back to previous page  
Copyright © 2008 GKISSANGA All rights reserved.