USHUHUDA WA MTOTO
USHUHUDA WA MTOTO FATUMA HAMISI MASUNGA (TZ-216-0223) Mtoto huyu alizaliwa tarehe 17/10/1995 kwa sasa yuko darasa la SABA katika shule ya MSINGI NKUHUNGU DODOMA TANZANIA. Ufuatao ni ushuhuda wake mwenyewe alio uandika tarehe 05/04/2008 Kwa jina naitwa Fatuma Hamisi Masunga. Kwanza kabisa naanza kwa kumshukuru Mungu kwa kuwa kuniwezesha kuwa hapa Kituoni, kwani maisha yangu yalikuwa magumu kwangu na familia yetu na sikudhani hata kama nitasoma.Mama yangu alikuwa anafanya biashara ya kuuza nyanya na akiuza ndipo tule. Baba yangu alikuwa anaumwa sana hadi alifikia kipindi hakawa haoni. Nakumbua siku ambayo niliandikishwa tulikuwa tumekwisha kunywa chai tumekaa nyumbani ndipo mwalimu alipo kuja kutuandikisha mimi na pacha mwenzangu. Kwa kweli tulifurahi sana kwani tulijua tumekwisha saidiwa. Nakumbuka baada ya kuandikishwa Kituoni tuianza kupewa vitu mbalimbali zikiwemo nguo, viatu na vingine vingi kama sabuni na mafuta. Namshukuru Mungu kwa sababu kaweza kuniunganisha katika maisha mazuri kwa kweli tunayo furaha sana. Pia baada ya uandikishwa tulianza kuja Kituoni kila siku za Jumamosi na kufundishwa masomo ya dini (Biblia). Masomo hayo yamenisaidia sana kutubadilisha maisha yetu. Ninashukuru sana Compassion kwani imeweza kunisaidia sana mimi pamoja na familia yangu kwa juma. Kwa sasa tumekuwa hatuna shida ya nguo, mafuta, viatu, hata madaftari.Ninamshukuru sana Mungu kwa yale yote aliyo nifanyia. Kwa kupiti Compassion kwa maana nimeweza kukombolewa maisha yangu. Pia napenda kuwashukuru wale wote pamoja na waalimu kwa kunisaidia. Sina mengi ya kusema kwani kwa sasa masomo yangu ni mazuri hata kwa darasa nililo fikia sasa niko darasa la saba bado miezi michache niweze kuhitimu masomo yangu. Nina mshukuru sana Mungu kwani kila siku ananibariki katika maisha yangu pamoja na familia yangu. Pia nina washukuru wale wote walio weza kunisaidia. Mungu aendelee kuwa bariki wawe na upendo huo huo. Asanteni Ni mimi Mtoto Fatuma Hamis Masunga. |
|||
Back to previous page |