USHUHUDA WA MTOTO

Home Contact Guest Book

 

       
       
 

USHUHUDA WA MTOTO CHRISTINA SAMSON MPILIMI (TZ-216-0069)

Mtoto huyu alizaliwa tarehe 02/08/1994 kwa sasa yuko Form one katika shule ya KIZOTA SEKONDARI DODOMA TANZANIA.

Ufuatao ni ushuhuda wake mwenyewe alio uandika tarehe 05/04/2008

Kwa jina naitwa Christina Samson Mpilimi ninamshukuru Mungu kwa kunifikisha mahali hapa kwani bila nguvu za Mungu nisingeweza kuwa hapa nilipo. Kwani kabla ya sijaanza kusoma hapa Kituoni TZ-216 ELCT NKUHUNGU STUDENT CENTRE nilikuwa naishi pamoja na wazazi wangu wote wawili kaka yangu pamoja na dada zangu wawili. Tulikuwa tukiishi kwa furaha sana katika familia yetu mimi nikiwa ni mtoto wa mwisho Nilipo kuwa darasa la tatu (STD III) Baba yangu alifariki hivyo tukabakia na mama tu ambae nae pia alifariki mwaka 2006. Lakini mama kabla hajafariki tulitafuta nyumba ambayo tuliweza kuinunua ndipo tulipo anza maisha mengine kabisa.

SITASAHAU siku ambayo niliandikishwa Kitoni kwani siku hiyo tulikuwa nyumbani tumekaa akatokea mama Ester na kuja kutuambia kuna sehemu wanaandikisha watoto ili wawasaidie. Ndipo mama yangu alipo inuka na kunileta Kituoni lakini tulipo fika na kuwauliza kama wanaandikisha watoto wakasema nafasi zimejaa, lakini mama yangu hakukata tamaa akaenda kuonana na Mchungaji. Na Mchungaji alimuambia mama ataandika jina langu kama akiba tu kama ikitokea nafasi basi ataniandikisha.Tukaendelea kusubiri mpaka pale walipo tangaza majina ya watoto ambao wataandikishwa rasmi likiwemo na jina langu. Tulimshukuru sana Mungu. Basi tukaanza taratibu za kuandikishwa na kuanza kuhudhuria Kituoni kila siku Jumamosi asubuhi pamoja na kujifunza neno la Mungu.

Kuwapo Kituoni nimefaidika na mambo mengi  kwani nisingeweza kusoma kwani dada yangu alikuwa hana uwezo wa kunisomesha shule ya msingi hata sekondari. Na nisingeweza kuwa na maisha ambayo niliyo nayo sasa. Ninamshukuru Mungu sana kwani kwa sasa naweza kupata mahitaji yangu karibu yote ya msingi mfano mahitaji ya shule kama Ada, sare, madaftari nk.

Ninamshukuru Mungu sana niliweza kufaulu darasa la saba na na kuingia kidato cha kwanza. Hivyo kwa sasa niko kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Kizota - Dodoma. Matarajio yangu ya baadae ni kuwa MWANASHERIA wa kutetea haki za watoto na wanawake.Naomba Mungu anisaidie ili malengo yangu yatimie

SHUKURANI: Nawashukuru  waalimu wangu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika maisha yangu ya kila siku na Mungu azidi kuwa bariki AMINA.

Ni mimi Mtoto Christina Samson Mpilimi.

 
  Back to previous page  
Copyright © 2008 GKISSANGA All rights reserved.